Mtihani Kenya
Download Android App
Download Our Apps to Access More Resources
Mwalimu Resources Pro Kiswahili Fasihi 102/3: KCSE Revision Kit
Pop-Up Subscription Notification
Maswali na Majibu ya Nguu za Jadi
MASWALI YA MARUDIO - RIWAYA YA NGUU ZA JADI

MASWALI YA MARUDIO; RIWAYA YA NGUU ZA JADI

1.
"Mtemi Lesulia alitegemea jasho la raia ili kujinufaisha pamoja na mabarakala wenzake.Kama mchwa, raia walijenga kichuguu kwa mate yao.Usiku na mchana walijituma.Hata walipomaliza kujenga, kamwe hawakustaladhi na kubarizi katika kivuli chake.Walienda mbio kulisha aila ya mtemi.Walihangaika ili kusitiri pato la nchi ambalo kiasi kikubwa kiliwaendea wenye vyao na vyeo nchini.Mtemi, kama mjusikafiri juu ya kichuguu aliingia katika shimo moja hadi jingine akiotea vyakula vya mchwa au hata kuwala mchwa wenyewe.Alinasa kila aina ya mdudu aliyeingia au kutoka katika vishimo vya kichuguu.Alikaa juu ya kichuguu akiota jua na kupigapiga kichwa chini kwa kujiamini kwamba ndiye mmiliki wa kichuguu.Mchwa kwake ni akina nani?"
a) Taja na ueleze aina nne za taswira zinazojitokeza kwenye kifungu. (alama 4)
b) Eleza mbinu nyingine za lugha zilizotumika katika dondoo. (alama 4)
c) Jadili changamoto inayopitia jamii inayoashiriwa kuwa "mchwa" kutokana na uongozi mbaya kwa kurejelea riwaya Nguu za Jadi. (alama 12)
2.
"amekuja hapa kwa sababu za kibiashara.Kifo cha panzi furaha ya kunguru ati. Mnajua ana kiwanda cha sharubati? Kesho mtamwona ameagiza vinywaji mbalimbali viletwe hapa muuziwe. Huenda akafungua kijiduka uchwara hapa."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Jadili sifa za msemaji wa maneno haya. (alama 4)
(c) Bainisha mbinu mbili za kimtindo kwenye dondoo. (alama 2)
(d) Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 10)
3.
"Mwenyezi Mungu ni mwema. Alisikia maombi na kilio chetu. Wanadamu wengine ni maadui wakubwa..."
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 2)
c) Eleza sifa mbili za msemaji zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
d) Jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari katika dondoo hili. (alama 12)
4.
(i) Tambua mbinu zozote nane za kimtindo katika dondoo hili. (alama 8)
"Very true. Uchumi wa nchi umewatia wengi taflisi. Viongozi wamevimba kichwa. Ninayosoma yote haya katika mitandao ya mawasiliano nikiwa huko ughaibuni.Wamewaacha watu kutumbukia mashimoni na washikilia kukutu kwamba wasalie humo". "Wamehiari kuwafukarisha ili wazidi kuwatawala. Dunia ya walalaheri hii. Chuma chao ki motoni. Tusubiri tu. Wengine watapigwa na bumbuazi wasalie kuokota taka mitaani." Aliongeza "Wapi! Wengi wao wataabiri vyombo wakimbilie ughaibuni. Watuachie sisi gofu la nchi tusalie kuchinjana tu," alitamka Lombo kwa huzuni. Kisha alimtazama Mashauri kwa muda na Kusema, "Tell me the truth, do you think babangu atashinda? Naonaamekumbwa na pingamizi nyingi. Wapinzani wake..."
ii. Jadili umuhimu wa mandhari ya Ponda Mali katika riwaya Nguu za Jadi. (alama 7)
iii. Jamii ya Matuo katika riwaya ya 'Nguu za Jadi' imekumbwa na usaliti si haba. Kwa kutoa Mifano mwafaka riwayani, onyesha ukweli wa kauli hii. (alama 5)
5.
"Asante kwa ushauri wako. Lakini ujue kwamba avaaye kiatu ndiye ajuaye kinapompekecha. Mahasidi wale kutupangia maovu kila dakika. Leo ni haya, kesho ni mengine. Dhuluma hii lazima ikomeshwe. Na sisi wenyewe ndio tutaikomesha. Tusitegemee serikali."
a) Weka dondoo hii katika muktadha wake (alama. 4)
b) Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya (alama. 3)
c) Tambua mbinu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hii (alama. 2)
d) Eleza mbinu zilizotumiwa na wananchi wa Matuo kukomesha dhuluma mbalimbali dhidi yao
e) Jadili umuhimu wa hotuba ya Lonare baada ya kuteuliwa kama kiongozi wa nchi ya Matuo (alama. 6)
6.
a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo (alama. 6)
Kuna waliookota chupa za plastiki kwenda kuchuuza. Kuna waliobobea katika kuchakura taka ili kupata mikebe iliyotupwa. Kisha waliichuuza mjini. Ukifika majaani, kitu cha kwanza kinachokukaribisha ni harufu kali ya uvundo uliosambaa kila mahali. Kila dakika magari yaliyosaki taka kutoka katika mitaa ya mji yalifika hapa ktupa taka. Mafalahi waliochoka na maisha waliishi mahali hapa. Walisitiriwa na makombo ya vyakula kutoka jaa hili kuu. Walinyanganyana chakula na kunguru waliojaa mahali hapa.
b) "Ibilisi wa mtu ni watu." Jadili ukweli wa kauli kwa kurejelea riwaya Nguu za Jadi (alama. 14)
7.
a) Changanua mtindo kwenye kifungu hiki (alama 5)
... alijitoma kwenye mabanda hayo yaliyosaki walevi nyakati hizi za jioni. Kelele zilizokuwa humo zingeweza kumtia mtu kichaa. Wengine waliimba ilhali wengine walipaaza sauti hata hungesikia walichosema. Baadhi yao nishai za ulevi ziliwapanda. Wakawa wanacheza kwa miondoko mbalimbali isiyoenda sambamba na nyimbo za santuri. Kuna baadhi ambao walikuwa wakilia na kutiririkwa na machozi bila kujua kilichowaliza. Hapa na pale kuna waliomkonyezea... na kumpigia mbinja... Alijifanya hawaoni ilmradi akamilishe usakaji wake. Alihisi kinyaa, akatamani apakimbie pahali pale. Lakini hakuwa ametimiza lililompeleka huko. Alihari kuyapitia yote bora ampate aliyemtafuta.
a. Ukirejelea dondoo hili, dondoa sifa zozote tano na mrejelewa. (alama 5)
b. "Maisha ya mrejelewa yalijaa kinyaa na mateso." Jazili mikakati aliyotumia kukabiliana na hali hii. (alama 10)
8.
a) "Ukosefu wa malezi bora una athari kwa jamii." Thibitisha kwa kurejelea riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 8)
a) "Ai! Faragha ya nyani imeishia ngokoni. Sasa wanafanya nini hawa hapa saa hizi? Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari ukirejelea riwaya nzima (alama 12)
9.
Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata:
"kama ni mila,basi leo nitaivunja.Kwanza hiyo usemayo ni ya kishenzi mno.Si ya maendeleo hata kidogo.Na ikiwa nyumba inateketezwa na moto mke hawezi Kwenda kumtafuta mumewe huko anakobarizi?mmm,niambie.Ikiwa mtoto ni mgonjwa mahututi,mke hawezi kwenda kumtoa mumewe ulevini akamhudumie mwanawe?"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Bainisha toni ya msemaji. (alama 2)
c) Eleza umuhimu wa msemewa wa dondoo hili. (alama 6)
d) Eleza umuhimu wa madhari wa dondoo hili. (alama 4)
e) Eleza namna msemaji alivyohusika katika kuvunja mila za jamii. (alama 4)
10.
Watategemewa na nani maishani? Hiki ndicho kizazi cha kesho au kizazi kilichopotea tayari?
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
b) Tambua toni katika mazungumzo haya. (alama 2)
c) Onyesha ni vipi kizazi cha leo na cha kesho kilivyopotea. (alama 12)
11.
Fafanua ufaafu wa anwani ya ‚ 'Nguu za Jadi '. (alama 20)
12.
Sasa alifahamu fika kwamba mzigo huo kamwe hauchukuliki. Fedheha ikamshika, uso ukamshuka. Sasa mambo yakamtokea puani.
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Fafanua umuhimu wa anayerejelewa katika kujenga riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 6)
c) Bainisha mbinu mbili za kimtindo katika dondoo. (alama 2)
d) "Sasa mambo yakamtokea puani." Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea msemaji na wahusika wengine wenye hulka kama zake. (alama 8)
MASWALI YA MARUDIO - RIWAYA YA NGUU ZA JADI
13.
(a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo. (alama 8)
Hakujua liliko bahasha ambayo ingemfungulia milango ya heri. Pengine ingemtoa katika maisha yale ya kujikunakuna. Ingemfanya kujua namna atakavyojenga duka jingine na kumwingiza katika pepo ya furaha daima. Haidhuru atakuwa amewaendea kinyume watu wake aliowapenda. Lakini ni lipi lisilowezekana mbele ya pesa? Kwanza nani angejua amepokea malaki hayo na kwa sababu gani? "Aah, potelea mbali," aliwaza, "Siku hizi kila mtu anazisaka chapaa, haijalishi ni kwa njia gani ilimradi maisha yamnyookee." `Kisha alisita na kusema kimoyomoyo, "Utu? Kwani mtu atakula utu. Inafaa mtu ajijenge kwanza kwa njia yoyote ile kisha afikirie masuala ya utu baadaye. Au hata aungame baadaye. Mungu si Athumani. Atamsikiliza na kupokea msamaha wake. Nani asiyeiba au kupokea mlungula siku hizi? Mimi sitakuwa wa kwanza wala wa mwisho."
(b) Fafanua jinsi vijana walivyosawiriwa riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 12)
14.
a) Riwaya ya Nguu Za Jadi ni kioo cha nchi za Afrika. Fafanua. (alama 20)
15.
........... alifanya kazi yake kwa moyo wa kujituma. Hakunung'unika pale kazi zilipomzidi bali alitabasamu na kuchapa kazi. Matatizo ya nyumbani yalipomzonga, hakukosa kufika kazini. Alidunduiza vijisenti vichache ambavyo alikuwa akipokea kama ujira wake akaweza kuwasomesha wanawe.
a) Tambua muktadha wa dondoo. (alama 4)
b) Fafanua sifa nne za msemewa. (alama 4)
c) Jadili changamoto za kikazi zinazojitokeza katika riwaya ya Nguu Za Jadi. (alama 12)
16.
"Mhn, ati familia? Kwani mimi mjinga niache mapesa haya yote yanipite bila kuyafaidi. Kipato ni hicho...kidogo hata hakiwezi kuilisha jamaa yangu kwa juma moja.Potelea mbali. Mangwasha na wanawe watajipanga. Pombe ya bwerere siachi ng'o! Najua Sagilu alimpenda sana Mangwasha wakati mmoja. Lakini si sasa.Hana haja naye.Kwani akina Sihaba wako wapi? Aah Mrima, vunja mifupa ukiwa bado una meno bwana."
(a) Changanua mtindo katika kifungu hiki. (alama 5)
(b) Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya. (alama 5)
(c) "Dunia ni tambara bovu...bovu sana. Ukivuta utachana. Acha waende zao." Kwa kurejelea wahusika mbalimbali kwenye riwaya nzima, fafanua ukweli wa maneno haya. (alama 10)
17.
Hivyo, alitaka kubadili hali hata kama ilimaanisha kukitia kichwa chake kinywani mwa simba. Alitaka kuliokoa jahazi lililokuwa likielekea mwambani kwa kasi. Lakini angeliweza vipi kupambana na utandu wa mahasidi hao?.
a) Eleza mbinu nne za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili (alama 4)
b) Eleza sababu za msemaji kutaka kufaulisha kauli iloyopigiwa mstari (alama 10)
c) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika kuijenga riwaya hii (alama 6)
18.
Dunia yote inajua aliyemsaliti Yesu Kristo. Unajua mtu huyo aliishia wapi?
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Tambua mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
c) Fafanua namna wahusika walivyowaendea kinyume wenzao katika riwaya ya Nguu za Jadi.
19.
'Wapi wengi wao wataabiri vyombo wakimbilie ughaibuni.Watuachie sisi gofu la nchi.Tusalie kuchinjana tu',
a. Eleza mkutadha wa nukuu (alama 4)
b. Fafanua umuhimu wa mnenaji (alama 6)
c. Vijana ndio wana uwezo wa kuikomboa jamii kutokana na utawala wa kiimla uliopitwa na wakati. Jadili haya kwa kuirejelea Riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 10)
20.
Mtemi Lesulia aliweka misingi kabambe kuakikisha kuwa hataweza kutimuliwa na wapinzani wake ili aendelee kuitawala Matuo maisha yake yote. Fafanua (alama 20)
21.
"Kwa miaka mingi ... alikuwa akikusanya mzigo wa miba. Sasa alifahamu fika kwamba mzigo huo kamwe hauchukuliki. Fedheha ikamshika uso, uso ukamshuka. Sasa mambo yakamtokea puani."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Kwa kutoa hoja kumi, jadili namna mrejelewa alikusanya mzigo wa miba. (alama 10)
c) Jadili namna mambo yanamtokea puani mrejelewa. (alama 6)
22.
Lingewahakikishia wenyeji wa Matango haki yao. Haki waliyokuwa wakipokwa mbele ya macho ya serikali. "Hakika atupaye tope hujichafua mwenyewe.... Watakimbia huku na huko kama wehu. Watavikimbia hata vivuli vyao."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 6)
b) Tambua vipengele vinne vya kimtindo kwenye dondoo hili. (alama 4)
c) Kwa kurejelea matukio kwenye riwaya, dhibitisha kuwa atupaye tope hujichafua mwenyewe. (alama 10)
23.
"Mimi ni mwanamume .Ninaweza kuoa wakati wowote na idadi yoyote ya wanawake. Mwanamke akishaolewa, basi yake yamekwisha hapo. Azae na kuitumikia jamaa yake bila kuulizauliza maswali.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. [alama 4]
b) Eleza sifa nne za msemewa wa maneno haya. [alama 4]
c) Eleza jinsi mnenewa alivyoitumikia jamii yake. [alama 6]
d) Jadili maudhui matatu yanayojitokeza kwenye dondoo hili. [alama 6]
24.
(a) Changanua mitindo katika kifungu hiki. [alama10]
Toka mbele yangu. Kwenda! Waketwa ni watu wasio na akili hata ya kuchagua wachumba. Ndivyo maana daima mnabaki nyuma kama makoti.Hata sijui kwa nini nilikuajiri. Umenivunjia heshima kumkataa rafiki yangu. Toka! Chifu Mshabaha alimfukuza Mngwasha kutoka afisini mwake. Kwa muda, Mangwasha hakujua kwa nini chifu mshabaha alimkaripia kiasi hicho. Alifululiza hadi kwake nyumbani. Alijifungia chumbani akalia kwa kwikwi. Alidhani chifu yule tayari alikwisha kumpiga kalamu. Hangeweza kumfukuza vile kisha amtake kurudi kazini. Alihisi kwamba Maisha ya uchochole sasa yanamkodolea macho. Aende wapi kwingine? Kazi hiyo ilimkidhia lishe na mavazi. Sasa angeshika mti gani?
a) Wakati jamii inapojitahidi na kupiga hatua,kuna watu ambao huwaendea wenzao kinyume. Jadili kwa hoja kumi ukerejelea riwaya nguu za jadi. [alama 10]
25.
'au amekuja hapa kwa sababu za kibiashara. Kifo cha panzi furaha ya kunguru ati. Mnajua anakiwanda cha sharubati? Kesho mtamuona ameagiza vinywaji mbalimbali viletwe hapa muuziwe. Huenda hata akafungua kijiduka uchwara hapa.'
a. Weka maneno haya kwenye muktadha wake. (alama 4)
b. Kwa kutumia mifano minne, jadili mtindo wa dondoo hili. (Alama 8)
c. Tathmini umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (Alama 8)
26.
'Mwanamke ni mhusika mkuu katika kuibomoa jamii yake.' Jadili. (Alama 20)
27.
"...Aliona jinsi raslimali ya nchi ilivyokuwa ikifujwa na watu walioshabikia wizi''
a. Eleza muktadha wa nukuu (alama 4)
b. Fafanua umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili (alama 4)
c. Bainisha toni katika dondoo hili (alama 2)
d. Jadili mbinu ishi zilizotumiwa na mrejelewa kupambana na hali katika kauli (alama 4)
e. Onyesha ukweli wa kauli iliyokolezwa wino katika nukuu (alama 6)
28.
Alishangaa barua hiyo iliingia vipi mle ndani. Kwa nini .......... aweke barua yake ndani ya mkoba wake bila kuisoma? Au alisahau alipokwenda zake uhamishoni? Na ilitoka wapi hasa? .........aliamua kuifungua bahasha, liwe liwalo. Potelea mbali hata kama haikuwa yake ........... mwenyewe alikuwa kesha mtema kama masuo. Barua ile ina maana gani kwake sasa hata akiisoma? Alijaribu kuitatanua ili gundi iachilie ule upeto wa juu wa bahasha lakini wapi. Gundi ilikazana kumsumbua hadi akaamua kuirarua raru raru bahasha ili mradi aifikie ile barua. Alikuwa mwangalifu asiirarue hata hivyo barua aliyotamani sana kuisoma. Aliichomoa akaona ilikunjwa peto tatu. Aliikunjua huku mikono ikitetemeka. Vidole vilijaa jasho kwa shauku ya kutaka kujua yaliyoandikwa. Iliandikwa kwa wino mweusi uliokoza.
a) Tambua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Changanua mtindo katika kifungu hiki. (alama 10)
c) Fafanua sifa za wahusika wanaorejelewa. (alama 6)
29.
"Lazima amejiunga na kundi la marafiki wenye pesa wanaojaribu kumpotosha."
a) Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
b) Anayesema maneno haya ni jasiri. Thibitisha kwa hoja tano. (alama 5)
c) Tathmini kwa hoja kumi na moja nafasi ya wenye pesa katika kuendeleza tamaa na ubinafsi katika nchi ya Matuo. (alama 11)
30.
"Mangwasha siku zote hizi ulikuwa unachezeshwa kayamba tu. Ati walisema Osama alikuwa hatari kwa usalama duniani; kuna Osama kuliko huyu?" alijiskia kusema. Alishusha pumzi kwa nguvu akajiuliza kimoyomoyo kwa nini Mungu aliruhusu moto kumtia kwenye shimo la maangamizi na wanawe. Hata hivyo, aliamini kuwa wakati mwingine Mungu huruhusu mabaya kutokea ili kuwafunza waja. Waaidha, alijua kuwa mashaka yanapomkumba mja, huwa ni funzo pia. Humtayarisha kuyahimili machungu zaidi ulimwenguni ama kumuasa dhidi ya kuabudu maovu. Maovu yanapotendwa na wachache, hata wale wasio na hatia pia hujikuta wamo humo uovuni. Ni mtego wa waliomo na wasiokuwemo.
a) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 5)
b) Eleza umuhimu wa mandhari ya kanisani aliko Mangwasha katika kukuza Riwaya ya Nguu za Jadi (alama 5)
c) Nchi ya matuo imeshinikizwa na Nguu Za Jadi zinazorudisha nyuma usawa katika jamii. Tathmini kauli hii kwa hoja kumi. (alama 10)
31.
"...amesalia gofu! Kakonda hata ukimpulizia pumzi ataanguka. Kasalia kamba ya mbuzi mwenzangu. Mchafu kama fungo. Amelewa chakari, hatazamiki."
a) Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
b) Tambua toni inayojitokeza katika dondoo. (alama 2)
c) Fafanua sifa sita za anayerejelewa katika dondoo (alama 6)
d) Ubinafsi ndio chanzo cha maovu ya kijamii. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea riwaya ya Nguu za Jadi (alama 8)
32.
. "Asifanye hivyo kwa nini? Ukuni mbaya haufichiki. Kigeugeu yule asiyenifaa kitu. Lumbwi yule,"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Fafanua dhima ya vipengele viwili vya kimtindo vinavyobainika katika dondoo hili (alama 4)
c) Fafanua umuhimu wa msemaji katika kuijenga riwaya ya Nguu za Jadi (alama 6)
d) Eleza umuhimu wa mandhari yanayojitokeza katika dondoo (alama 6)
33.
"Dunia ni tambara bovu ... bovu sana. Ukivuta utachana.Acha waende zao."
a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b. Tambua mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili. (alama 2)
c. Fafanua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili. (alama 4)
d. Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kutumia mifano kumi maridhawa riwayani. (alama 10)
34.
"Samahani... Nina shida kidogo. Ninaomba usaidizi. Sikuwa nikilipa ushuru katik biashara zangu. Sasa wanataka kuzifunga na kunipeleka kotini."
a. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
b. Bainisha toni katika dondoo hili (alama 2)
c. Msemaji wa maneno haya na wengine ni adui ya wananchi wa Matuo. Eleza ukweli wa kauli hili. (alama 14)
35.
Matumizi mabaya ya mamlaka ni tatizo sugu sana katika mataifa mengi ya Afrika yanayoendelea kiuchumi. Kwa kutolea hoja mwafaka, tetea ukweli wa kauli kwa mujibu wa riwaya ya nguu za jadi. (alama 20)
36.
"Ha! Tangu lini mwanamke akawa na machache. Mna maneno mengi kama chiriku."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
b) Bainisha mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili. (Alama 4)
c) Tambua toni ya msemaji katika dondoo hili. (Alama 2)
d) Ndoa nyingi katika jamii zinakumbwa na changamoto si haba. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea Nguu za Jadi. (Alama 10)
37.
Au amekuja hapa kwa sababu za kibiashara. Kifo cha panzi furaha ya kunguru ati......
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Bainisha mbinu mbili za kimtindo zinajitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
c) Fafanua umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 6)
d) Thibitisha ukweli wa maneno yaliyopigiwa mstari kwa kurejelea riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 8)
38.
"Mbona mbio hivyo mwenzangu? Umefuguzwa?"
a. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b. Onyesha kwa kutolea mifano mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili (alama 2)
c. Fafanua jinsi mwandishi wa riwaya ya Nguu za Jadi ameshughulikia swala la utamaduni. (alama 14)
39.
"Unataka kuwaita polisi? Hee heeee! ... Unafikiri mapenzi yanaogopa polisi?"
a. Fafanua vigezo vitatu vilivyotumiwa kumpa msemaji wa maneno haya sifa zake (alama 3)
b. Msemaji wa maneno haya ni mwenye tamaa na ubinafsi. Jadili (alama 7)
c. Fafanua jinsi utawala mbaya wa Mtemi Lesulia ulididimiza maisha ya wananchi wa Matuo (alama.10)
40.
''Hakujua akimbilie wapi. Sasa afanye nini? Alilitupia lile jinyama lakini likahepa. Alihisi maisha yake yamo hatarini.''
a. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b. Tambua mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
c. Fafanua namna wahusika walivyowaendea kinyume wenzao katika riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 12)
41.
Mnanipa pole kwani nimefiwa na nani? Kwani mlidhani nitasalia kuwa mtemi wenu siku zote za maisha yangu? Nimechoka ati. Ndiyo maana sikutaka kushinda.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
b) Kwa kurejelea riwaya eleza jinsi wananchi hawa walivyojikomboa kutoka kwa uongozi wa mtemi huyu? (alama 10)
c) Eleza sifa zozote sita za anayezungumza (alama 6)
42.
Ushindi wake Lonare uliashiria mwamko mpya kwa wananchi wa Matuo. Kwa kutoa mifano mwafaka jadili matarajio hayo. (alama 20)
43.
a) "Ikiwa mmoja wa hawa wenzangu atadhurika, nitamwaga mtama. Liwe liwalo."
i. Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
ii. Eleza athari nne za msemaji kumwaga mtama ukirejelea riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 4)
b) "Hivyo ndivyo ulivyofunzwa na mamako? Ama kweli, wanawake wa kisasa wanavunja kila mwiko uliowekwa na wazee." Kwa hoja kumi na mbili, thibitisha ukweli wa kauli iliyopigwa mstari ukirejelea riwaya Nguu za Jadi. (alama 12)
44.
a) Changanua mbinu za kimtindo katika dondoo hili. (alama 6)
"Hata huyo Lesulia unajuaje atakuwa mtemi wetu tena? Umeishi ndani ya kivuli cha Lesulia kiasi cha kwamba hujui uchaguzi unabisha? Umo ndotoni wewe! Aliye juu msubiri chini, kaka. Wavyele hawakukosea waliposema ulichokiacha pwani, kakingoje ufuoni."
a) Tathmini ukweli wa kauli hii ukurejelea riwaya Nguu za Jadi. (alama 14)
45.
Mrima alikuwa akitabaradi kwenye ndoto zake, hana habari wala taarifa. Mkewe aliamua kumwita kwa nguvu huku akimfinya sikio. Mrima alihisi maumivu, akafunga jicho moja akasema, "Nikilaala.... shida i...ko wapi? Kwendeeni huko.... Ma...loofa nyie." Waliamua kumwinua. Walimbeba hobelahobela hadi kwenye gari. Alikuwa hatamaziki. Uchafu wa siku nyingi ulimfanya kunuka kama kisonzo. Nywele zilisokotana. Meno yalipiga manjano kutokana na ugaga uliokolea. Alivaa nguo bwaga mtwae tu. Nguo hizo zilicheua harufu mbaya mithili ya kicheche. Mangwasha chozi la huzuni lilimdondoka. Mrima alilalama huku akitoa matusi lakini hakuna aliyemsikiliza. Lonare aliamua kumpeleka hospitali moja kwa moja.
(a) Changanua mtindo katika kifungu hiki (alama 10)
(b) Jadili umuhimu wa mandhari ya Majaani kwa kurejelea riwaya nzima (alama 4)
(c) Tambua toni inayodhihirika katika maneno ya Mrima (alama 2)
(d) Eleza umuhimu wa mhusika Mangwasha ukirejelea dondoo hili (alama 4)
46.
"Lakini mbona umeamua kunyamaza hivyo? Huoni watu wanakutegemea?" "...Wajua, kinywa kilichofumbwa hakiingii nzi."
a) i. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5)
ii. Tambua toni katika dondoo hili. (alama 2)
iii. Taja mbinu moja ya lugha katika dondoo kisha utoe mfano wa mbinu hii katika dondoo. (alama 2)
a) Mataifa mengi ya bara Afrika yanakumbwa na matumizi mabaya ya mamlaka ambayo ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya kiuchumi.Kwa kutolea mifano kumi na moja riwayani ya 'Nguu za Jadi',tetea ukweli wa kauli hii. (alama 11)
47.
"Ndugu zangu, ukabila ni sumu ya nyoka. Ukabila huangamiza maendeleo ya nchi hata kama imestawi kiasi gani."
a) Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
b) Eleza umuhimu nne wa msemaji wa kauli hii. (alama 4)
c) Onyesha mbili za uandishi zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
d) Kwa kutumia hoja zisizopungua kumi, jadili maudhui ya ukabila yanavyojitokeza katika riwaya hii. (alama 10)
48.
"Waite. Unadhani mapenzi yanaogopa polisi"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Fafanua sifa sita za msemewa (alama 6)
c) Kwa kutoa mifano taja mbinu tatu za kimtindo katika dondoo hili (alama 3)
d) Msemewa na wenzake ni adui wa wananchi wa Matuo. Fafanua ukweli kauli hii kwa kurejelea riwaya ya Nguu Za Jadi (alama 7)
49.
"Nikupe ushauri dada.Kaa mbali naye kwani Yule ni moto wa kuotewa mbali. Ukimfuatafuata,anaweza kukutendea mambo mabaya"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Tambua mbinu za kimtindo zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
c) Andika sifa nne za "dada" anayetajwa na msemaji katika dondoo hili. (alama 4)
d) Jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari. (alama10)
50.
a) Chambua mtindo. (alama 8)
Walitembea kuelekea mahali hapo kwa muda wa nusu saa.Mwishowe,waliona korongo kubwa.Ndanimwe,mlikuwa na walevi waliolala fofofo.Walikuwa wakipokezana mikoromo mizigo mizito iliyowashtua kina mama wale.Walijua lazima Mrima angekuwa hapo.Walipitapita huku wakiwakaguanyuso. Hakuna uso uliofanana na ule wa Mrima.Mangwasha akazidi kufadhaika.Alikuwa na uhakika kama mchana kwamba angemkuta mumewe mahali hapo.Wakaamua kwenda katika upande wa pili wa korongo hilo.Hapa pia palikuwa na walevi waliolewa chakari.Baadhi yao walikuwa wanavuta sigara.Wengine waliendelea kubugia pombe kutoka katika chupa walizobeba.Wengine tayari walikuwa wametekwa na usingizi.Walilala vinywa wazi bila kujali nzi waliong'ong'a nyuso zao.Lonare ndiye aliyemtambua Mrima. Alikuwa amelala kifudifudi,kaegemeza kichwa kwenye gogo.Lonare alimsukasuka ili aamke lakini wapi. Mrima alikuwa akitabaradi kwenye ndoto zake,hana habari wala taarifa.Mkewe aliamua kumwita kwa nguvu huku akimfinya sikio.Mrima alihisi maumivu,akafungua jicho moja na kusema," Nikilaala...shida i..iko wapi? Kwendeeni huko...ma...loofa nyie."Waliamua kumwinua.Walimbeba hobelahobela hadi kwenye gari.Alikuwa hatazamiki. Uchafu wa siku nyingi ulimfanya kunuka kama kisonzo.Nywele zilizosokotana.Maneno yalipiga manjano kutokana na ugaga uliokolea.Alivaa nguo bwaga mtwae tu.Nguo hizo zilicheua harufu mbaya mithili ya kicheche.Mangwasha chozi la huzuni lilimdondoka.Mrima alilalama huku akitoa matusi lakini hakuna aliyemsikiza.Lonare aliamua kumpeleka hospitali moja kwa moja.Hali yake ilihitaji matibabu ya dharura.Matibabu ya mwili na akili.
a) Jadili umuhimu wa mandhari ambamo kifungu hiki kimenukuliwa. (alama 12)
51.
"Nisikilize Chaurembo. Tena unisikilze vizuri sana. Wakati mmoja nilitaka sana kukuoa. Nawe ukaringa ukamkimbilia kijana yule mpuuzi, mlevi na ..."
a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b. Fafanua sifa za Msemewa katika dondoo hili. (alama 8)
c. Eleza umuhimu wa Madhari ya nyumbani kwa msemewa katika kujenga riwaya ya Nguu za Jadi. (alama. 8)
52.
a) Tambua mbinu zozote sita za kimtindo katika dondoo hili. (alama 6)
"Very true. Uchumi wa nchi umewatia wengi taflisi. Viongozi wamevimba kichwa. Ninayosoma yote haya katika mitandao ya mawasiliano nikiwa huko ughaibuni. Wamewaacha watu kutumbukia mashimoni na washikilia kukutu kwamba wasalie humo" Aliongeza Lombo. "Wamehiari kuwafukarisha ili wazidi kuwatawala. Dunia ya walalaheri hii. Chuma chao ki motoni. Tusubiri tu. Wengine watapigwa na bumbuazi wasalie kuokota taka mitaani." Aliongeza Mashauri. "Wapi! Wengi wao wataabiri vyombo wakimbilie ughaibuni. Watuachie sisi gofu la nchi tusalie kuchinjana tu," alitamka Lombo kwa huzuni. Kisha alimtazama Mashauri kwa muda na Kusema, "Tell me the truth, do you think babangu atashinda? Naona amekumbwa na pingamizi nyingi. Wapinzani wake..."
a. "Jinsia ya kiume imedhulumiwa katika riwaya ya Nguu za Jadi" Eleza (alama. 14)
53.
(a) "Karibu mwenzangu.Subiri nikuletee kikombe cha chai..." "Hata usilete,sina hamu ya chai mwenzangu.Nina machungu moyoni.Ndiposa nimekuja unisaidie kuyapunguza.... Kuyamaliza hutaweza"
i. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
ii. Jadili nafasi chanya na hasi ya mwanamke katika kuendeleza riwaya ya Nguu za Jadi. (alama16)
54.
(a) "Kuna kitu kinachoendelea baina ya watu hawa wawili. Lakini ni kitu gani hicho kinachoweza kuwaleta mahasimu wale pamoja?"
i. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
ii. Fafanua sifa nne za anayezungumza maneno haya. (alama 4)
iii. Eleza mbinu moja ya kimtindo kwenye dondoo. (alama 2)
(b) Onyesha jinsi usaliti unavyoshughulikiwa katika riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 10)
55.
Aidha, ngome inapoteketezwa na waovu wachache walio ngomeni, hawatasalia wale wasio na hatia. Msiba huwaendea wote.
a) (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama. 4)
(ii) Jadili namna mrejelewa anavyoendeleza na kukuza vipengele vifuatavyo. Ploti (alama 3) Wahusika (alama 3)
b) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 10)
"Pengine maneno yako yana ukweli kidogo" "Si kidogo. Huu ndio ukweli mtupu. Huu ndio uhalisi wa mambo. Ukweli daima hupendeza kila wakati, ingawa huweza kuwa mchungu pia. My brother, wewe ukitaka kuona penzi usitafte mjini. Nenda kijijini. Huko utabahatika kupata huba. Lakini ujitayarishe kumfundisha ustaarabu wa mji. Umfunze hata kutumia vitu kama microwave, hee hee hee!" Aliendelea kucheka. Meno yake yalijaa papachi. Inashangaza kwa nini mtemi na mapesa yote yale hakumpeleka kwa daktari wa meno. Angalau aondoe hizo papachi kinywani.
56.
'Suluhisho ni kwamba hayo mahema yapelekwe Matango... Hatuhami hata kwa makombora.'
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza sifa nne za msemaji. (alama 4)
c) Fafanua umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. (alama 4)
d) Fafanua mikakati ambayo msemaji na wenzake walitumia kukabiliana na hali zao katika nchi ya Matuo. (alama 8)
57.
a) Changanua mtindo katika dondoo hili. (alama 6)
'...hakuwa na hamu ya kuzikimbilia zile noti wala kuchota zile sarafu. Alipozitazama,zilimtafishi na kumtia kichefuchefu.Hapo alipata nafasi ya kulikimbia na kujisalimisha.Jinamizi hilo lilimshtua sana hadi akaamka.Mwili wote uliloa jasho.Alijaribu kulala tena lakini akashindwa kabisa.Hapo ndipo aliposikia mayowe mfululizo.Kuna nini?Alifungua dirisha la chumba chake akatazama nje.Mama yangu!
b) 'Lazima tuokoe kizazi hiki kinachopotea nyikani bila matumaini.'
i. Msemaji wa kauli hii amedhihirisha uwajibikaji mkubwa katika jamii. Thibitisha. (alama 7)
ii. Jadili changamoto zinazowakumba wananchi kwa kurejelea hotuba ya Lonare katika Uga wa Taifa. (alama 7)
58.
a) Baada ya Lonare kushinda uchaguzi na kuwa Mtemi wa Matuo alinuia kuzingatia hatua kadhaa ili kujenga upya nchi ya Matuo. Eleza (alama 10)
a) "Ujinga wa kutotambua kwamba kile walichoiba ndicho kitakachowatia kitanzi." Onyesha ufaafu wa usemi huu kwa kurejelea Riwaya nzima. (alama 10)
59.
a) "Lazima amejiunga na kundi la marafiki wenye pesa wanaojaribu kumpotosha."
i. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
ii. Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya. (alama 6)
b) Matatizo yanayowakumba wanamatuo ni mwiba wa kujidunga. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea Nguu za Jadi. (alama 10)
60.
Kamwe hangekubali kuwa mtu wa kuomba omba misaada na ufadhili kutoka kwa wale walio navyo. Aliumbwa mkamilifu, akili timamu na siha mwilini. Kwa nini basi aombe wale waliokirimiwa vitu kama yeye? Ni ada ya binadamu kufanya kazi ili aweze kulisukuma gurudumu la maisha.
a. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b. Bainisha toni katika dondoo hili. (alama 2)
c. Fafanua maudhui katika dondoo hili. (alama 3)
d. Eleza sifa tatu za anayerejelewa kwa kurejelea riwaya ya Nguu za Jadi. (alama 8)
e. Fafanua jinsi wahusika mbalimbali kwenye riwaya ya Nguu za Jadi wanavyofanikisha kauli iliyopigiwa mstari. (alama 8)
61.
(a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo. (alama 6)
Kuna waliookota chupa za plastiki kwenda kuchuuza. Kuna waliobobea katika kuchakura taka ili kupata mikebe iliyotupwa. Kisha waliichuuza mjini. Ukifika majaani,kitu cha kwanza kinachokukaribisha ni harufu kali ya uvundo uliosambaa kila mahali. Kila dakika magari yaliyosaki taka kutoka katika mitaa ya mji yalifika hapa kutupa taka. Mafalahi waliochoka na maisha waliishi mahali hapa. Walisitiriwa na makombo ya vyakula kutoka katika jaa hili kuu. Walinyanganyana chakula na kunguru waliojaa mahali hapa.
b) Bainisha toni inayojitokeza katika dondoo hili. (Alama 2)
c) Jadili mbinu walizotumia raia wa Matuo kujikomboa kutokana na uongozi dhalimu wa Mtemi Lesulia. (Alama12)